BLOG

Taarifa kwa Umma

 Washindi wa Tuzo za Digitali (Tanzania Digital Awards) Watangazwa.

                       02nd October 2021, Dar es Salaam, Tanzania.

Washindi wa kwanza wa Tuzo za Kidigitali (Tanzania Digital Awards) mwaka 2020 wametangazwa rasmi baada ya watanzania kupiga kura. Jumla ya wawania Masoko Mtandao, Burudani Mtandaoni, Vyombo vya Habari Mtandaoni Uvumbuzi wa Kidijitali, Mawasiliano ya Kidijitali, Uchechemuzi Mtandaoni na Tuzo ya Ujumla ya Chaguo la Watu.

Tuzo hizi zilizinduliwa nchini kwa mara ya kwanza mnamo Januari 16, 2020 kwa lengo la kutambua juhudi za watu binafsi, mashirika, kampuni na hata Serikali katika kutumia teknolojia ya kidigitali kuleta mabadiliko chanya katika jamii. Baadhi ya walioshinda vipengele vingi ni pamoja na Diamond Platnumz ambaye ameshinda vipengele vitatu ikiwemo kipengele cha Tuzo ya Ujumla, Msanii bora wa mwaka na mraghibishi wa mwaka. Millard Ayo pia ametwaa tuzo tatu, tuzo ya kiongozi bora wa vyombo vya habari vya mtandaoni, TV bora ya Mtandaoni na Blog bora ya Mtandaoni.


Taasisi zilizonyakua tuzo nyingi ni pamoja na Ubongo Kids na Idara ya Uhamiaji kila mmoja tuzo mbili. Ubongo Kids wametwaa tuzo tuzo ya ukurasa bora wa elimu mtandaoni na tuzo ya aplikesheni bora ya elimu mtandaoni. Idara ya Uhamiaji wametwaa tuzo ya uvumbuzi bora kupitia huduma yao ya kutoa hati ya kusafiria kielektroniki. Uhamiaji pia wameshinda tuzo ya taasisi bora ya Serikali mtandaoni.

Vodacom Tanzania imeibuka na tuzo mbili baada ya aplikesheni yake ya M-PESA kuzawadiwa kama Aplikesheni Bora ya Huduma za Kifedha. Tuzo nyingine iliyoenda kwa Vodacom ni tuzo ya Kampeni Bora ya Masoko Mtandaoni ambapo Vodacom wameshinda kupitia kampeni yake ya Yajayo Yanafurahisha.

Tuzo ya heshima imekwenda kwa Muhidin Issa Michuzi ambaye ametambuliwa kama kiongozi bora wa vyombo vya habari mtandaoni kwa kuanzisha na kuendeleza vyombo vya habari kwa njia ya mtandao nchini Tanzania.