Phone : +255 737 957082      Email : info@digitalawards.co.tz

BLOG





Msimu wa Tuzo za Kidigitali Tanzania (Tanzania Digital Awards) kwa mwaka 2022 umezinduliwa rasmi Jumanne, Disemba 13, 2022 jijini Dar es Salaam. Tuzo hizo zilizoanzishwa na Serengeti Bytes zinalenga kukuza uwajibikaji, ubunifu, na uvumbuzi katika matumizi ya teknolojia za kidigitali nchini Tanzania.

 

Msimu wa kwanza na wa pili wa tuzo za Tanzania Digital Awards ulipata mwitikio mzuri kutoka kwa wadau mbalimbali na Watanzania kwa ujumla. Zaidi ya mapendekezo 60,000 yalipokelewa huku kura 250,000 zikipigwa kutoka kwa wananchi, kuchagua washindi 108 katika vipengele mbalimbali.

 

Taasisi za umma, makampuni, mashirika yasiyo ya kiserikali na watu binafsi walipendekezwa na kupigiwa kura katika vipengele vikuu 12 katika msimu wa mwaka 2021. Vipengele vikuu vilivyoshindaniwa mwaka jana ni pamoja na Serikali Kidigitali, Diplomasia Kiditali, Masoko na Biashara Kidigitali, Burudani Kidigitali, Vyombo vya Habari Kidigitali, Uvumbuzi wa Kidigitali, Mawasiliano Kidigitali, Uchechemuzi Kidigitali, Benki Kidigiitali, Mawasiliano ya Simu Kidigitali, Tuzo ya Chaguo la Watu na Tuzo ya Heshima.

 

Kwa mwaka 2022 Tanzania Digital Awards imeendelea na idadai ya vipengele vikuu 12 na vipengele vidogo 52 kama inavyobainishwa hapa chini:

 

Kipengele cha Uvumbuzi Kidigitali kina vipengele vidogo nane:

- Mvumbuzi wa Kidigitali wa Mwaka

- Uvumbuzi wa Kidigitali katika Kilimo

- Uvumbuzi wa Kidigitali katika Afya

- Uvumbuzi wa Kidigitali katika Elimu

- Uvumbuzi wa Kidigitali katika Haki

- Uvumbuzi wa Kidigitali katika Usafirishaji

- Uvumbuzi wa Kidigitali katika sekta ya Fedha na Benki

- Uvumbuzi wa Kidigitali katika Sekta ya Vyombo vya Habari

 

Kipengele cha Benki Kidigitali kina vipengele vidogo vinne:

- Benki ya Mwaka

-  App bora ya Benki

- Benki Bora katika Uvumbuzi wa Kidigitali

- Huduma Bora kwa Wateja

 

Kipengele cha Mawasiliano ya Simu Kidigitali kina vipengele vidogo vinne:

- Kampuni Bora ya Mawasiliano ya Simu

- Huduma Bora kwa Wateja

- App Bora ya Huduma za Kifedha

- Kampuni Bora ya Mawasiliano ya Simu katika Uvumbuzi

 

Kipengele cha Mawasiliano Kidigitali kina vipengele vidogo vitano:

- Muunda Maudhui Bora.

- Mraghibishi Bora.

- Mpiga picha Bora.

- Mbunifu wa grafiki wa mwaka.

- Muandaa Video Bora.

 

Kipengele cha Burudani Kidigitali kina vipengele vidogo sita:

- Msanii Bora Kidigitali (Mwanaume).

- Msanii Bora wa kidigitali (Mwanamke).

- Klabu Bora ya Mpira wa Miguu Kidigitali.

- Mwanamichezo Bora Kidigitali.

- Mchekeshaji Bora Kidigitaliwa (Mwanamke)

- Mchekeshaji Bora Kidigitali (Mwanaume).

 

Kipengele cha Msoko na Biashara Kidigitali kina vipengele vidogo saba:

- Kampeni Bora ya Masoko Mtandaoni.

- Mjasiriamali Bora Kidigitali (Mwanaume).

- Mjasiriamali Bora Kidigitali (Mwanamke)

- Chapa Bora ya Kitanzania Mtandaoni.

- Kampuni Bora ya Huduma za Masoko Mtandaoni.

- Kiongozi Bora wa Biashara Kidigitali (Mwanamke).

- Kiongozi Bora wa Biashara Kidigitali (Mwanaume).

 

Kipengele cha Vyombo vya Habari Kidigitali kina vipengele vidogo sita:

- TV Bora ya Kidigitali

- Blogu ya Mwaka

- Kampuni Bora ya Vyombo vya Habari Kidigitali

- Redio ya Mtandaoni ya Mwaka

- Mwanahabari Bora Kidigitali (Mwanamke)

- Mwanahabari Bora Kidigitali (Mwanaume)

 

Kipengele cha Serikali Kidigitali kina vipengele vidogo vitano:

- Mwanasiasa Bora Kidigitali (Mwanaume)

- Mwanasiasa Bora Kidigitali (Mwanamke)

- Shirika Bora la Serikali Kidigitali

- Uvumbuzi Bora Katika Utoaji wa Huduma za Kijamii

- Chama Bora cha Siasa Kidigitali

 

Kipengele cha Uchechemuzi Kidigitali kina vipengele vidogo vinne:

- Shirika lisilo la kiserikali lenye matumizi bora ya mitandao

- Kampeni Bora ya Uchechemuzi kupitia Mitandao ya Kijamii

- Kiongozi Bora wa shirika lisilo la kiserikali kidigitali (Mwanaume)

- Kiongozi Bora wa shirika lisilo la kiserikali (Mwanamke)

 

Kipengele cha Diplomasia Kidigitali kina vipengele vidogo vitatu  

- Ubalozi/Shirika la Kidiplomasia Bora Mtandaoni

- Kiongozi wa Kidiplomasia wa Mwaka Mtandaoni (Mwanaume)

- Kiongozi wa Kidiplomasia wa Mwaka Mtandaoni (Mwanamke)

- Shirika Bora la Kimataifa Kidigitali

 

Tuzo ya Chaguo la Watu

 

Tuzo ya Heshima

 

Uzinduzi wa msimu wa 2022 umekwenda sambamba na kuzinduliwa kwa mchakato wa kupendeleza wawania tuzo. Mchakato umepangwa kuanza tarehe 13 hadi 27 Desemba 2022. Mchakato wa mapendekezo utafanywa kupitia fomu ya mapendekezo inayopatikana kwenye tovuti ya Tanzania Digital Awards. Wadau na kila mmoja ana uwezo wa kupendekeza watu wanaoweza kuwania tuzo hizo katika kipengele kinachofaa. Watu binafsi, makampuni na watu binafsi wanaweza kujipendeka katika vipengele mbalimbali kutokana na sekta zao.

 

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo jijini Dar es Salaam, Michael Mallya, Afisa Uendeshaji wa kampuni ya Serengeti Bytes – ambao ni wandaaji wa tuzo hizo amesema misimu miwili iliyopita ya tuzo hizo imekuwa na ushindani wa hali ya juu na wa kusisimua hivyo wanatarajia tuzo hizo kuwa na msisimko zaidi mwaka huu.

 

“Tangu kuzinduliwa kwake mwaka 2020 Tuzo za Tanzania Digital Awards zimekua na kuongeza thamani katika ekolojia ya teknolojia za kidigitali nchini. Mwaka jana tuliona msimu wa kusisimua na wenye ushindani. Tuliongeza vipengele vikuu viwili zaidi kufuatia mapendekezo ya wadau mbalimbali. Lengo la kuongeza vipengele ni kuongeza ushirikishwaji wa sekta ambazo tayari zinafanya vizuri kupitia teknolojia za kidigitali. Kufuatia kuongezeka kwa uelewa juu ya tuzo hizi tuliona kuongezeka kwa ushirikishwaji na ushiriki wa umma na wadau wengi zaidi katika msimu uliopita. Kutokan na mchango wa tuzo hizi kwa watu binafsi, taasisi na taifa kwa ujumla katika kukuza mageuzi ya kidijitali nchini Tanzania, tunatarajia msimu huu utakuwa mkubwa zaidi.” Amesema Mallya.

 

Mallya ameeleza mpango mzima wa Tuzo za Tanzania Digital Awards. Amesema baada ya mchakato wa uteuzi mapendekezo, kamati ya ufundi ambayo ina jukumu la kufanya tathmini itawachuja wateule kwa kila kipengele na majina yatawekwa kwenye tovuti kwa ajili ya kupiga kura kuanza tarehe 5 - 26 Januari 2023. Baada ya kukamilika kwa mchakato wa kupiga kura, kamati ya kiufundi itafanya tahtmini ya kura na kuidhinisha washindi tayari kwa hafla ya tuzo ambayo imepangwa tarehe 25 Februari 2023.

 

“Kila msimu wa TDA una ladha yake ya kipekee. Katika misimu miwili iliyopita, hatukuweza kuwakutanisha wadau na washindi kwa tukio la tuzo kwa sababu kama vile COVID-19 na nyinginezo ambazo zilikuwa nje ya uwezo wetu. Licha ya hayo, washindi walisheherehekewa mitandaoni na tuzo zilitolewa kwa kila mshindi. Msimu huu tunafuraha kutangaza kuwa tutafanya hafla ili kuwaleta pamoja mabingwa wa kidijitali na wadau mahsusi wote ili kusherehekea mafanikio ya mageuzi ya kidijitali nchini,” amesema Mallya.

 

Wananchi na wadau wanahimizwa kutembelea tovuti ya Tanzania Digital Awards (www.digitalawards.co.tz) kwa taarifa zaidi kuhusu vipengele, vigezo, upendekezaji, upigaji kura na udhamini. Kwa maelezo ya ziada, unaweza kuwasiliana na waandaaji kupitia barua pepe info@digitalawards.co.tz/partnerships@digitalawards.co.tz au kupitia simu kwa nambari +255 737 957 082.

 

Tanzania Digital Awards zilianzishwa Januari 16, 2020, kwa lengo la kutambua mchango wa watu binafsi, makampuni na taasisis zinazotumia teknolojia za kidigitali kuhamasisha uvumbuzi, ubunifu na uwajibikaji katika maendeleo kwa ujumla.